Hatua Kwa Hatua Jinsi ya Kutengeneza Blog (Wavuti) Bure

Kufungua Blog ni bure na hakuna malipo ya aina yoyote. Unaweza kutengeneza Blog kwa kutumia simu, Computer au Tablet.  

Muhimu

Inabidi utumie jina la pekee ambalo mtu akiitafuta jina la blog ya iwe ya kwanza kwasababu hii itawarahisishia wasomaji waitafute blog yako kwa urahisi kupitia jina. Siyo mtu anasearch jina la blog yanatoka majina kama 100 hivi halafu hata jina la blog yako halitokei. Mwanzoni nilitumia jina la agatha64 lakini ukisearch kwenye Google blog yangu haitokei kwahiyo nikatumia agath64a. Kabla ya kutengeneza blog yako ingia kwenye Google kisha andika jina unalotaka kutumia. Hii husaidia sababu kuna mwingine utamwambia ingia kwenye blog yangu ya agath64a utaona kuna post inayozungumzia kutengeneza blog kama atakutana na majina 100 ya majina ya watu itakuwa ngumu kuipata blog yako.


Hatua Kwa Hatua Jinsi ya kutengeneza website/blog (Wavuti)

1. Unatakiwa uwe na email ya Gmail Ili uweze kutengeneza blog au kama unayo email lazima iwe active. Ingia kwenye website ya Gmail ili uweze kutengeneza email

2. Ingia kwenye website ya blogger.com kisha Sign up ili uweze kutengeneza blog. Itafunguka ukurasa kama wa kwenye picha chini hapo. Bonyeza create your blog itakuomba email. Weka email na password


3. Title: Weka jina la blog yako (andika jina lolote unaloona linafaa). Hakikisha jina halipatikani au halijawahi kutumia kwenye kutengeneza blog. Weka Jina ambalo ni rahisi kwa wasomaji wako kuitafuta blog yako

Address: Andika jina la blog yako mfano maharagwembeya.blogspot.com hakikisha jina la kwenye address halifanani na jina la address ya blog yoyote ile dunia. Hakikisha ukisearch jina la blog yako itatokea yenyewe tu

Themes: Chagua yoyote unayoona inafaa. Kisha bonyeza kitufe cha Create blog. Hapo utakuwa umeshamaliza kutengeneza blog yako. Na itaonekana kama hivi


Jinsi ya kubadilisha jina la blog (wavuti) yako

Baada ya kutengeneza blog yako unaweza kubadilisha jina lolote lile unalotaka lakini baada ya kubadilisha huwezi kurudisha jina lile la kwanza. Unaweza kubadilisha blog title na address muda wote. Ingia kwenye website yako, settings kisha bonyeza Basic, Title >>> Edit. Blog Address Edit


Jinsi ya kufuta blog temporarily (Kwa muda ) au permanently (wakati wote). Kabla ya kufuta blog yako unashauri ubackup kwanza post zako. Kumbuka ukifuta blog yako permanent hairudi na huwezi kutumia jina hilo tena kutengenezea blog nyingine.

1. Ingia kwenye blog yako. Bonyeza settings kisha Other. Bonyeza Delete Blog



Jinsi ya kuedit Profile kwenye blog yako

Ingia kwenye blog yako. Bonyeza Settings kisha User settings. Bonyeza User Profile kisha Edit



Jinsi ya kuandika Article na kupost kwenye blog yako

1. Ingia kwenye Blog yako. Bonyeza Posts kisha New Post


2. Baada ya kumaliza kuandika. Bonyeza Labels kuchagua sehemu gani post yako inataka kukaa kulingana na mada. Unaweza kuzitengana Post zako kulingana na mada zenyewe mfano Computer, Modem na Software Kisha bonyeza Done. Bonyeza Publish na Post yako itaonekana kwenye blog yako


Jinsi ya kuweka Link (Url) kwenye post ya blog yako

Highlight neno unalotaka kuliwekea link. Kisha Bonyeza Link. Kwenye Web Address, weka url yako. Weka tiki kwenye Open file in a new window kama unataka ifungukie kwenye new window


Jinsi ya kubadilisha / kuconvert blog yako kuwa application ya android apk na iPhone IOS bure bila kuwa na ujuzi wowote

1. Ingia kwenye website ya Gonative. Weka Url ya blog yako mfano https://agath64a.blogspot.com. Kisha bonyeza Build >>

2.  Where should we send the link? Weka email yako kisha bonyeza build my app!. Subiri kama dakika 5 app yako itakuwa tayari


3. Ingia kwenye email yako na click link kama inavyooneka kwenye picha ili uweze kudownload app yako

Nimekuandalia kitabu ambacho kitakusaidia kutengeneza Blog (wavuti) bure ambapo utaweza:-
Pia nimekuwekea Blog premium template ambapo utaweza kuiweka kwenye blog yako. 

11 comments:

  1. Mtu anawez kuona vip posti zangu na link yangu

    ReplyDelete
  2. Nimefurahishwa sana na maelezo yako maana nimefanikiwa kupata nilichokihitaji kwa urahisi zaidi. Ongeza bidii na kazi njema

    ReplyDelete
  3. nikihitaj zaidi mawasiliano nakupataje

    ReplyDelete
  4. Nakuomba tuwasiliane simu 0767654924

    ReplyDelete
  5. Nimepata muangaza kidogo kwani hamu yangu ni kutengeneza blog.

    ReplyDelete
  6. Nashukuru kwa darasa lako nmi hamu yangu ni mimi kumiliki blog lakini nina simu sna kompyuta inawezekana naomba nijulishe kwenye namba yangu hii 0687056380

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.