Mambo ya kuzingatia unapojifunza ufundi simu
Mambo muhimu ya kuzingatia unapojifunza ufundi simu
1. Operating System
Unatakiwa ujue Operating system inayotumika kwenye computer yako. Ni windows 7, 8, 8.1 au 10 na bit gani yaani ni x86 au x64. Hii itakusaidia kufanya mambo yafuatayo kwenye computer yako
-Jinsi ya kudisable driver signature
-Jinsi ya kuinstall drivers za simu kwenye computer yako
2. Bootloader
Huu ni mfumo unaowekwa kwenye simu ili kuendesha simu yako. Pia hutumika kufunga simu yako ili mtumiaji asiweze kubadilisha kitu chochote kwenye simu kama vile kuweka mfumo mpya wa toleo la simu. Kuunlock bootloader kwenye simu ingia settings-About Phone. Bonyeza Build number mara saba mpaka uambiwe "You are now a developer". Ikishaandika bonyeza kitufe cha back. Utaona neno Developer options. Bonyeza hapo. Kisha weka on kwenye "Enable OEM unlock", kisha weka on USB debugging. Tumia Adb kuunlock Bootloader. Kuna baadhi ya simu kama Huawei utatakiwa kuingia kwenye website zao ili kuomba Code. Kila Simu ina mfumo wake wa kuunlock. Ingia YouTube kujifunza zaidi. Uzuri simu nyingi hazijafungwa bootloader
3. Device chipset (Mobile's CPU)
Unatakiwa ujue simu inatumia chipset gani ni
1. MTK
2. SPD
3. RDA
4. MSTAR
5. QUALCOMM
Jinsi ya kujua Device chipset ya simu yako. Hii itakusaida kuchagua tool gani utumie kwenye simu kutatua tatizo kulingana na Device cheapset kama vile kuflash simu, kutoa lock, kuroot, kuunlock simu zinazotumia mitandao mmoja na n.k
4. Secure Boot
Ni mfumo wa ulinzi unaowekwa kwenye simu ili kukuzuia kubadilisha mfumo wa simu kama vile kuroot, kuunlock n.k. Simu yenye Secure boot haikupi uwezo wa kuangalia mafile ya system yaliyoko kwenye file manager kama vile Blootooth n.k
-Download Secure Boot Download Agent (DA) File
-Jinsi ya kuflash DA file kwenye simu yako
5. ROM
Hapa unatakiwa ujue kuwa kuna Stock na Custom Rom
Stock Rom
Hii zinatengenezwa na kampuni husika mfano Tecno, Samsung, Itel, Xiomi, Vodafone, Alcatel
Custom Rom
Hizi zinatengenezwa na mtu binafsi kulingana na mahitaji yake kwahiyo anaweza kuongeza muonekane wa themes, kutoa apps au kuongeza n.k Ili uflash simu yako ni lazima u-root na unlock bootloader kwenye simu kwanza tofauti na hivyo utaua simu yako
Kwahiyo utaweza kuflash simu kulingana na jina la simu na model yake mfano kuna Tecno F1, Tecno S2 kwahiyo hizi simu haziingiliani stock firmware.
6. Boot key
Kila simu ina boot key iwe Feature phone (Simu za button) au smartphone. Boot key hutumiaka pale unapoflash simu, kurepair imei, kutoa Lock n.k kwenye simu yako.
-Jinsi ya kujua boot key kwenye simu za button
-Jinsi ya kujua boot key kwenye simu za smartphone
-Jinsi ya kuboot simu kwenye recovery mode
7. Tools
Unatakiwa ujue ni tools gani zinatumika kulingana na device chipset za simu. Kuna Tool za bure na zingine za kulipia
MTK - Splash tool (Tecno, Zte, Vodafone, Baadhi ya Itel (Feature phone) n.k Hautakiwi kukariri maana watengenezaji hubadilisha CPU
SPD - Upgrade au research (Simu za Itel, Samsung (Feature phone), Alcatel n.k
Symbian na Java - Nokia PC Suite na Phoenix
Samsung smartphone - Odin
iPhone - iTunes, 3utools
Sony - Xperia flash tool
LG - RSDALite na LG flash Tool
Motorola - Motorola flash tool
Hizi box zinauzwa ila bei yake inaanzia 300,000. Unaweza kutumia crack zinafanya kazi bila ya box ila siyo 100%
NCK
MIRACLE BOX
GSM ALADDIN
OCTOPLUS
Z3X-SAMSUNG NA LG
FURIOUS GOLD
CHIMERA
BST DONGLE
SGIMA KEY
INFINFITY BEST
MRT DONGLE
Jiunge na magroup ya WhatsApp ya mafundi simu ili uongeze maarifa zaidi
HARDWARE
Jiunge
SOFTWARE
Jiunge
HARDWARE & SOFTWARE
Jiunge
Important Notice
Kuna solution nyingi sana zipo mtandaoni kwahiyo unatakiwa uwe uperuzi kila wakati kwasababu kila muda teknolojia inabadilika. Utakutana na vitu vipya vinavyohusu Bootloader, Secure boot, rooting, Flashing, Unlocking, Frp (Factory reset protection) n.k
Kuna forum nyingi kama vile mundebatech, Hovatek, gsmhosting na Youtube
Post a Comment