Jinsi ya kushare file za 4shared, Mega na Google drive

Hizi ni Cloud Storage kama vile unavyohifadhi data zako kwenye flash drive, Memory card, Hard disk, au DVD lakini hii njia inahitaji internet. Kama una picha, video na Document muhimu. Zitunze kwenye Cloud Storage mojawapo kwa maana hata kifaa chako kikiharibika utazipata data zako popote na kwa kifaa chochote. Njia hii inatumika kwenye Simu, Computer, Tablet na Vifaa vingine 

Hizi Cloud Storage zinatoa 15GB bure ila kama una matumizi zaidi ya hapo inabidi ulipie

Faida

-Hii itahifadhi vitu vyako milele labda hiyo kampuni ifirisike
-Data zako zitakuwa salama zaidi. Hazitaharibika
-Utazipata popote pale utakapozihitaji

Hasara

-Kama matumizi yako ni zaidi ya 15GB utalipia
-Chochote utakachoupload kuna uwezekano wa wao kukiona
-Huwezi kupata data zako kama hauna kifurushi cha internet

Kuupload ni kitendo cha kutoa file kutoka kwenye computer au devices yoyote na kuviweka  kwenye Cloud Storage

Kudownload ni kitendo cha kutoa file kutoka kwenye Cloud Storage na kuviweka kwenye computer, simu, tablet au kifaa chochote. Ili kukamilisha mchakato wa ku-upload na ku-download lazima kuwepo na internet

File hujumuisha kitu kimoja kimoja mfano kitabu kimoja au unaweza kuzip na vitabu vingine ili kutengeneza file moja

Folder ni kama kapu lilobeba vitu vingi ndani yake. Unaweza kuwa na kitabu, programu, audio, video n.k

Fuata hatua hizi ili uweze kushare link za file zako na marafiki zako

4SHARED

1. Ingia kwenye website ya 4shared. Sign up kwa kutumia email yako. Unaweza kudownload bila ku-sign up. 

2. Bonyeza kwenye neno Upload ili uweze kuupload file zako kwenye 4shared


3. Kushare file kwa  marafiki zako lazima utengeneze link. Bonyeza kwenye hiyo icon mbele ya neno Share au right click utaona neno share kama unatumia computer.


3. Bonyeza kwenye kibox cha Shorten URL ili kutengeneza link


5. Copy hiyo link na share na marafiki zako


MEGA

1. Ingia kwenye website ya Mega kisha Sign up kwa kutumia email yako. Kuupload file au folder zako bonyeza kitufe cha File upload au Folder juu kulia mwa browser yako


2. Kushare file, Right click kwenye folder unalotaka kushare na watu wako. Kisha bonyeza Get link


3. Hiyo ndiyo link ya kushare na watu wengine. Bonyeza kitufe cha kucopy 


GOOGLE DRIVE

1. Ingia kwenye website ya Google Drive kisha Sign Up kwa kutumia email yako

2. Kuupload. Bonyeza kitufe cha New


3. Chagua unataka kuupload file au folder


2. Kushare. Right click kwenye file unalotaka kushare na watu wengine. Kisha bonyeza Get shareable link


3. Utapata ujumbe "Link copied to the clipboard". Hiyo ndiyo link ya kushare

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.