Jinsi ya kufufua Flash Drive, Hard disk na Memory card iliyokufa


Flash drive, Hard disk na Memory card zikiwa hazisomi huleta ujumbe wakukutaka u-format na uki-format inakuandika 'windows is unable to format" au unasikia mlio lakini ukienda kwenye my computer huoni partition ya flash drive, Hard disk au memory card yako

Hatua za kufuata ili uweze kufufua flash drive, Hard disk na memory card

Njia ya kwanza

1. Bonyeza window button + E kisha right click kwenye my computer au This computer kisha bonyeza Manage


2. Bonyeza Disk Management. Right click kwenye partition ya hard disk, memory card au flash drive. Chagua change drive letter and paths


3. Bonyeza change kisha chagua herufi kwenye kibox cha Assign the following driver letter kisha bonyeza OK.



Njia ya pili

Njia hii itakusaidia kuformat flash drive, memory card au hard drive yako pindi windows is unable to format

Flash drive na memory card

Jinsi ya kufufua Flash drive na Memory Card

1. Bonyeza window button + X kisha chagua command prompt (Admin)


2. Itafunga command Prompt.


Hapo andika maneno haya kwenye CMD
- Diskpart kisha bonyeza Enter
- List disk bonyeza Enter. Itakuonyesha list za disk zote kwenye computer yako. Chagua disk unayotaka kuformat yangu ni disk 1
- Select disk 1 bonyeza Enter
- Clean bonyeza Enter
- Create partition primary bonyeza Enter
- Select partition 1 bonyeza Enter
- Active bonyeza Enter
- Format fs=fat32 bonyeza Enter
- Exit bonyeza Enter

Mpaka hapa itakuwa tayari

Hard disk 

- Diskpart kisha bonyeza Enter
- List disk bonyeza Enter. Itakuonyesha list za disk zote kwenye computer yako. Chagua disk unayotaka kuformat yangu ni disk 1
- Select disk 1 bonyeza Enter
- Clean bonyeza Enter
- Create partition primary bonyeza Enter
- Select partition 1 bonyeza Enter
- Active bonyeza Enter
- Format fs=ntfs label=WC-Drive quick bonyeza Enter
- Assign letter=W Bonyeza Enter
- Exit bonyeza Enter

Jinsi ya kuformat computer yote

Hapa utaweza futa kila kitu kilichopo kwenye computer yako kuanzia doc, Audio, Video n.k mpaka windows utaifuta kwahiyo itakuhitaji kuinstall windows upya.

Hatua za kufuata

1. Zima computer yako
2. Washa computer yako na bonyeza SHIFT+F10 kwa pamoja bila kuachia
3. Itawaka kwenye CMD (Command Prompt). Andika haya maneno kwenye CMD
- diskpart bonyeza Enter
- list disk bonyeza Enter
- select disk 0 bonyeza Enter
- clean bonyeza Enter
- convert GPT bonyeza Enter
- Exit bonyeza Enter

2 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.