Jinsi ya kubadili Logo au picture kwenye nyimbo za Audio na Video


Sasa hivi kuna wimbi kubwa la kuwepo kwa Logo au picture kwenye music wowote ule unaodownload kwenye internet au kurushiwa kutoka kwa mtu. Utakuta kuna picha au logo zingine hazifai au huzipendi. Hii software itakuwezesha kufuta, kuweka kutokuweka logo au picha yoyote kwenye nyimbo za Audio au video.

Mahitaji

Download Audioshell

1. Baada ya kudownload ina kuinstall kwenye computer yako. Usiifungue. Ingia kwenye folder la music au video kisha right click kwenye nyimbo unaotaka kubadilisha logo au picture.

-Kama nyimbo ni mmoja bonyeza kwenye Tag Editor


-Kama nyimbo ni zaidi ya mmoja, bonyeza kwenye Multi Files Tag Editor. Kama nyimbo ni zote kwenye folder lako la nyimbo unabonyeza Ctrl + A kama ni baadhi ya nyimbo press and hold CTRL+ kisha unaclick kwenye nyimbo unazozitaka. Baada ya hapo unaachia ctrl kisha right click. Hapa picha itakuwa mmoja tu kwa nyimbo zote 


2. Bonyeza kwenye Remove button kuiondoa hiyo picha.


3. Bonyeza kwenye add button kuadd logo au picture


4. Hapa chagua picha au logo unayoitaka kisha double click au single click kisha bonyeza open


5. Bonyeza save button. Pia unaweza kubadilisha taarifa yoyote unayoitaka kwenye nyimbo au video


6. Nyimbo yako itaoneka hivi

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.