Jinsi ya kuona Password ulizozihifadhi kwenye browser yako

Hii njia inatumika kwenye computer ambapo itakuwezesha kuona Password ulizo Sign up au Sign in kwenye website mbalimbali kupitia browser ya Chrome na Mozilla

Mozilla Firefox

1. Ingia kwenye mozilla Firefox. Juu kulia kwenye browser yako. Bonyeza vimistari vitatu. Itakuja menu kama hapo chini. Bonyeza Options

2. Bonyeza Privacy & Security na kisha bonyeza Saved Logins
3. Bonyeza Show Passwords na kisha bonyeza Yes. Hapo utaona password zote ulizozihadhi kwenye browser yako ya Mozilla

CHROME

1. Bonyeza vidoti 3 juu kulia mwa browser yako. Menu itafunguka kisha bonyeza Settings


2. Bonyeza Passwords
3. Bonyeza kwenye kitufe cha Show Password kwenye account unayotaka kuona password. User name, Andika jina unalotumia kwenye computer na Password, weka Password unayotumia kusign in kwenye computer yako kisha bonyeza OK. Hapo utaweza kuona password zote zilizohifadhiwa kwenye Chrome.

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.