Jinsi ya Kutengeneza PDF File kwa Microsoft Office Word



Hii njia itakusaidia kutengeneza PDF file kwa kutumia Microsoft Office Word kwenye Computer yako. Kama unatumia Microsoft Office Word 2007, Download Save As PDF and XPS kwenye computer ili uweze kutengeneza PDF file kwa kutumia Microsoft Office Word

Fuata hatua hizi ili uweze kutengeneza PDF file kwa kutumia Microsoft Office Word kwenye Computer yako

1. Baada ya kuandika kazi yako kwenye Microsoft Office Word. Juu kushoto mwa Microsoft Office Word, bonyeza kwenye file


2. Kisha Save As na kisha browse ili kuchagua sehemu ya kuhifadhi kazi yako


3. Chagua PDF na kisha U-save kazi yako, sehemu unayoona inafaa kuhifadhi file lako


Jinsi ya kubadilisha PDF kwenda Microsoft Word Doc, Docx au Picha
 Jinsi ya kuweka Password kwenye File la PDF kwenye Microsoft Office Word

i. Bonyeza Options.


ii. Weka tiki kwenye Encrypt the document with a password



iii. Weka password ziwe tarakimu 6 au zaidi kisha bonyeza Ok


iv. Bonyeza Save kuhifadhi kazi yako.


Jinsi ya kuweka Password kwenye file la Microsoft Word Document (DOCX)

A. Bonyeza file >>> Info >>> Protect Document na chagua encrypt with password


B. Weka Password kisha bonyeza Ok


C. Rudia kuweka Password uliyoweka mwanzo ili kuhakikisha kama zinafanana na ya mwanzo, kisha bonyeza OK.


Kumbuka kuweka password utakayoikumbuka kwa urahisi kwasababu utakaposahau inabidi utumie Software itakayokuwezesha kubypass Password

Jinsi ya kutoa Password kwenye Microsoft Word Document (DOCX) yako unayoikumbuka.

- Fungua Document Word File, kisha fungua ukurasa mpya. Copy kazi yako na kisha ui-paste kwenye ukurasa mpya na kisha Save kazi yako.

Au tumia hii software kutoa password kwenye PDF file unayoikumbuka. Download Ipub-pdf-password remover

- Convert PDF file to Word. Download PDF to word Converter Offline. Kama unataka ubadilishe to Word online tumia PDF TO WORD CONVERTER ONLINE

- Kusoma PDF file zako tumia Sumatra PDF Reader ni nzuri sana

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.