Jinsi ya kuweka Subtitle kwenye Movie au Series yoyote


Kuna wakati unataka kuangalia movie au series ila ugumu unakuja kwenye lugha wanayotumia huenda wanatumia lugha ya kihindi, kichina, kikorea au lugha yoyote ile usiyoielewa. Sasa hapo inakuja ugumu wa kutafuta Subtitle na kuiweka kwenye movie yako. 

Fuata hatua hizi kuweka Subtitle kwenye Movie au Series yako. Hakikisha una kifurushi cha internet angalau cha 100mb. Njia nzuri na rahisi ni ya kutumia VLC Media Player na ALLplayer. You may also like Download Movie, Animation na Series nzuri wakati wote 

SIMU
Njia ya kwanza

VLC Media player

1. Download VLC apk and install kwenye simu yako

2. Open movie au series unayoitaka

3. Tap kwenye Screen utaona ki-icon kama cha kutuma meseji, bonyeza hapo kisha tap on download subtitle. Hakikisha simu yako imeungwanisha na internet. Baada ya sekunde kadhaa utaona Subtitle inaonekana kwenye movie au series yako



Njia ya pili

Websites
1. Ingia kwenye website ya Subtitle TVsubtitles.netwww.subscene.com, au www.freemoviesub.com, kisha download Subtitle inayoendana na format ya movie au series yako. Kwa series unadownload subtitle inayoendana na episode. Kama vile DVDrip, avi, xvdi, BRrip, Blueray, MP4, MKV, WEB n.k


2. Download Es file manager apk na install kwenye simu yako

3. Tumia Es file manager ku-extract file la subtitle uliyo-download. Utakuta file lako lina format ya srt

4. Nenda kwenye folder la Subtitile. Liandike jina sawa na movie au series yako. Mfano. Movie inaitwa Fallen Kingdom kwahiyo itakuwa Fallen Kingdom.srt na kwenye Series hivyo hivyo subtitle lazima iendane na jina la episode 

5. Kisha ihamishie Subtitle kwenye folder la movie au series yako. Kisha play movie yako au series utaona subtitle imeonekana kwenye movie au episode ya series yako

COMPUTER
Njia ya kwanza

ALLPLAYER
Hakikisha computer yako imeunganishwa na internet.

1. Download Allplayer na install kwenye computer yako. Tafuta movie au series unayotaka kuiangalia. Iplay hiyo Movie

2.  Right click kwenye Screen, kisha bonyeza kwenye Preferences. 


3. Click on Subtitles Server tab, kisha weka tick kwenye Automatically download subtitle na In case of missing subtitles, download the list of subtitles from openSubitles.org. Utaona subtitle imeanza kuoneka kwenye movie yako.


Njia ya Pili

VLC Media Player
1. Download VLC Media Player kisha install kwenye computer yako.

2. Fungua VLC Media PLayer na play movie au series yoyote.  Bonyeza kwenye View na kisha VLsub. 



3. Jina la Movie litatokea kwenye Title. Pia unaweza kuandika jina la movie yoyote au kupunguza jina la movie kama utasearch subtitle ukaikosa. Pia unaweza kuchagua lugha ya subtitle yako. Bonyeza Search by harsh
Au Search by name
4. Chagua Subtitle inayoendana na jina la movie yako kisha Bonyeza Download Selection. Baada ya sekunde kadhaa utaiona subtile kwenye Movie yako. 



Njia ya tatu

Website
1. Ingia kwenye website ya subtitle TVsubtitles.net,  www.subscene.com, au www.freemoviesub.com, na download subtitle inayoendana na format ya movie au series yako. Kwa series unadownload subtitle inayoendana na episode. Kama vile DVDrip, avi, xvdi, BRrip, Blueray, MP4, MKV, WEB n.k


2. Extract file lako kwenye computer (tumia winRar  au 7-zip ku-extract). Utakuta file lako lina extension ya srt

3. Lihamishe file lako wenye folder la movie au episode ya series unayotaka kuiangalia


4. kisha liandike jina sawa na movie au series (Episode) yako . Mfano. Movie inaitwa Fallen Kingdom kwahiyo itakuwa Fallen Kingdom.srt na kwenye series hivyo hivyo subtitle lazima iendane na jina la epsode au Right click katika movie wakati inaplay nenda subtitle then locate ilipo hiyo subtitle yako. Itaanza kuonekana kwenye Movie yako

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.