Jinsi ya kuipata simu iliyopotea au iliyoibiwa
Hakikisha Simu yako imeunganishwa na gmail na ina Play Store
Mahitaji
Download Android Device Manager apk
Kazi zake
-Itakuonesha sehemu ilipo simu yako
-Itafuta taarifa muhimu kwenye simu yako
-Italock au kuunlock pattern au password huko iliko
-Itaweza kupiga alarm kwa dakika 5 na kuendelea
-Itaweza kutrack simu popote pale
Hatua za kufuata ili uweze kujua sehemu ilipo simu yako
1. Tafuta simu ya Android
2. Download Android Device Manager apk na install kwenye simu yako
3. Fungua app ya Android Device Manager
4. Jaza Email na password ambayo umetumia kwenye Google Play Store
5. Itafute simu yako na utaoneshwa mahali ilipo simu yako
6. Utaona Option tatu baada ya kulog in kwenye Android Device Manager
-Ring (itapiga alarm sehemu ilipo)
-Lock (Utai-lock simu yako huko iliko)
-Erase (Itafuta taarifa zako zote kwenye hiyo simu
Tumia hizi app kwenye simu yako ili pindi ikibiwa itakuwa rahisi wewe kuipata simu yako
Njia hii itakusaidia kuona picha za mwizi wako. Hizi apps zitampiga picha mtu yoyote akikosea Password, Pattern au Pin kwenye simu yako.
Gesture Lock Screen
Download Gesture lock screen apk na install kwenye simu yako. Register app yako kwa email. Mtu yoyote akikosea pattern au password, itampiga picha na kukutumia kwenye email yako. Ukitaka kuziona picha, unaingia kwenye email yako utazikuta
2. CM Security App
Download CM Security App apk na install kwenye simu yako. Kisha ifungue na register kwa email. Ina sehemu ya ku-protect SMS, WhatsApp, Messenger na apps zingine kwa Password ili kumzuia mtu asitumie simu yako.
Mtu yoyoe akikosea Pattern, Pin au Password itampiga picha na kuituma kwenye email
3. Hiddeneye apk
1.Download Hiddeneye apk na install na kisha register kwa email yako. Ina alama ya jicho
2. Fungua app yako utaona neno juu limeandikwa Security status. Upande wa kulia kwenye hilo neno utaona neno off kwenye kibox. Click hapo ili kuweka On. Mtu yoyote akikosea password, Patter au Pin itampiga picha na kuituma kwenye email yako.
Post a Comment