Jinsi ya kupata kitabu chochote bure bila malipo yoyote
Hizi ni website ambazo zitakuwezesha kupata vitabu mbali mbali kulingana na mahitaji yako. Vipo vitabu vya story, uchumi, politics, comics n.k Hivi vitabu ni bure yaani hakuna malipo yoyote inayohitajika katika kupata hivi vitabu. Hivi vitabu vipo katika mfumo wa Pdf na Epub ili uweze kusoma lazima uwe na Sumatra PDF Reader au Adobe Pdf Reader Nakushauri download Sumatra kwa sababu ni bure na pia ukisoma kitabu, ukaishia chapter 2, siku ukihitaji kusoma tena itaanzia hapo hapo ulipoishia kusoma.
Zifuatazo ni website zitakazokuwezesha kupata vitabu mbali mbali bure bila malipo yoyote
Wikibooks
Hii ni website yenye vitabu vingi sana ambayo itakuwezesha kupata kitabu chochote bila malipo yoyote. Ingia Wikibooks na uanze kufurahia ulimwengu wa vitabu
Archive.org
Hii pia ni moja ya website nzuri sana kwa utoaji wa vitabu bure bila ya malipo yoyote. Ina vitabu vingi vya kila aina kuhusu siasa, uchumi, vichekesho n.k Ingia Archive.org uanze kufurahia ulimwengu wa vitabu
BookBub
Hii ni website itakayokuwezesha kupata vitabu kulingana na mahitaji yako. Vitabu vyote ni bure yaani hakuna malipo yoyote yanayohitajika. Ingia BookBub
Free-ebooks.net
Ni website nzuri kwa mahitaji ya vitabu mbali mbali kama vile siasa, story, vichekesho n.k. Ingia Free-ebooks.net uanze kufurahia ulimwengu wa usomaji wa vitabu
Amazon
Hii ni website iliyosheheni vitabu vingi vya siasa, uchumi, mapenzi, Psychology n.k. Vyote vyote vipo katika mfumo wa Pdf na epub. Ingia Amazon na uanze kusoma vitabu uvipendavyo
Africanbookscollective
Hii ni website iliyojaa vitabu kama ni mpenzi wa vitabu basi hii ni website bora kwa ajili yako.
Goodreads
Hii ni website nzuri ya vitabu. Ina vitabu vingi vilivyo kwenye fomart ya Pdf, mobi na epub. Vitabu vyote katika website hii ni bure yaani hakuna malipo yoyote
Post a Comment