Jinsi ya kuunlock modem ya huawei e3372h-153 ya Tigo Tanzania

Kuna matoleo ya e3372h mengi kwahiyo ni vizuri kuangalia modem yako inaishia na namba ngapi mwisho. Hii njia ni kwa modem ya e3372h-153 tu ya Tigo kwahiyo usitumie njia hii ku- unlock e3372h-510 Tigo au ku- Unlock e3372h-607 TTCL kwasababu utabrick modem yako na sitahusika kwa uharibifu wowote. Nimekutengenezea unlocking firmware kwa ajili ya kuunlock modem yako ya Huawei e3372h-153.

Specification za e3372h-153 ya Tigo

- Hardware version: CL2E3372HM

- Software version: 22.200.09.00.787

- Web UI version: 17.100.11.01.787

- Dashboard version : WEBUI_17.100.11.01.787


Mahitaji
- Transional Firmware 
- Modified Firmware
- Modified Web Interface
- Huawei Drivers
- DC Unlocker
- Huawei Unlock Code Calculator

Namna ya kufungua Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mtandao wowote
1. Chomeka modem ya E3372h-153 kwenye Computer yako ikiwa ina SIM Card ya mtandao mwingine kisha run Huawei drivers. Hii husaidia modem iweze kutambuliwa katika mchakato wa kuunlock modem
2. Fungua DC Unlocker exe, kisha Chagua "Huawei modems" kwenye Select Manufacturer na "Auto Detect" (Recommended) kwenye Select model kisha bonyeza magnifying glass button. 
Itakuletea information za modem yako. Taarifa za modem zako zitatokea ikiwa hazijatokea basi chomoa modem yako kisha chomeka tena kwenye computer. Hakikisha hakuna device nyingine iliyochomekwa zaidi ya modem ya Huawei E3373h-153
3. Fungua Huawei Unlock Code Calculator kisha weka IMEI za modem yako ambazo zipo 15. Baada ya kuweka bonyeza kitufe cha Calc ili kupata Flash Code. Kumbuka zinazohitajika hapo baadae hizo Flash Code
4. Install Transitional Firmware kisha bonyeza start. Iache mpaka imalize hatua zote na mwisho itakuleta alama ya vyema yenye kitufe cha kijani
5. Rudi kwenye DC Unlocker software. Bonyeza magnifying glass, itakuletea taarifa za modem yako. Mwisho wa taarifa ingiza hizi command AT^SFM =1 kisha bonyeza kitufe cha "Enter" kwenye keyboard ya computer yako
6. Run Modified Firmware kwenye computer yako, itakuomba Password. Weka za Flash Code ulizozipata kwenye Huawei Unlock Code Calculator kwenye hatua namba 3
7. Run Modified Web Interface kisha bonyeza Start. Iache mpaka imalize hatua zote zenyewe na mwisho itakuletea alama ya vyema yenye rangi ya kijani.
8. Rudi kwenye DC Unlocker software, Bonyeza Magnifying Glass button tena. Itakuletea taarifa za modem yako mwisho wa taarifa za modem yako ingiza hizi command AT^NVWREX=8268,0,12,1,0,0,0,2,0,0,0,A,0,0,0 kisha bonyeza
kitufe cha Enter kwenye keyboard ya Computer yako. 
Ikishamaliza basi Bonyeza Magnifying Glass button itakuletea taarifa za modem yako. Angalia kwenye SIM Lock Status itakuandikia Unlocked. Hongera umefanikiwa kufungua modem ya E3372h-153 na utaweza kutumia laini ya mtandao wowote ule unaoutaka.

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.