Jinsi ya kuwezesha COM Port ya Huawei Hilink Modem

Hizi ni modem ambazo zinafunguka kwa kutumia browser na mara nyingi port zake zinakuwa hazionekani kwenye Computer Management >> Decice Mager >>> Ports (COM & LPT). Com ports ni muhimu sana pindi tunapotaka kuunlock au kutumia third part software kwenye modem za Hilink.

MUHIMU

Kama unatumia Windows 64 bit (Jinsi ya kuangalia Windows bit ya computer yako kama ni X86 au X64inabidi u-disable Driver Signature Enforcement kwenye computer yako

Jinsi ya kuinstall COM Port of Huawei Hi-link Modem kwenye computer yako

NJIA YA KWANZA

1. Chomeka modem yako ya Hilink kwenye computer. Itafungua Browser yenye address hii http://192.168.1.1/

2. Isipofunguka basi tumia hii address. Weka kwenye Address bar kwenye browser yako. http://192.168.1.1/html/switchProjectMode.html au  http://192.168.8.1/html/switchProjectMode.html 

3. Ingia kwenye Device Manager kwa kubonyeza Window button + E button >> Right click kwenye My computer au This PC >>> Manage >>> Device Manage >>> Other devices

4. Right click kwenye Huawei Hilink kisha bonyeza kwenye Update Driver 

5. Bonyeza kwenye Search automatically for updated driver software.

6. Itaanza kuinstall Drivers za modem yako

7. Itaonekana kama hivi baada ya kuinstall drivers

8. Rudia hatua hiyo hiyo kwenye Huawei Hilink ya pili kuupdate driver

NJIA YA PILI

i. Chomeka modem yako kwenye computer kisha fungua browser na weka address hii http://192.168.8.1/

ii. Download na kisha run Switch Mode Script ili kuinstall drivers za modem yako

iii. Drivers zako zitakuwa kama hivi hivi

NJIA YA TATU

Mahitaji

Download Huawei Hilink Driver ewser2k

A. Ingia kwenye Computer Management kwa kuright click kwenye My Computer au This PC >>> Manage >>> Device Manager >>> Other Devices

B. Right click kwenye HUAWEI MOBILE >>>>>> Update Driver Software

C. Bonyeza kwenye Browse my computer for driver software

D. Chagua Let me pick from a list of drivers on my computer kisha bonyeza Next

E. Chagua Show All Devices, bonyeza Next

F. Bonyeza kwenye Have Disk kisha peruzi mpaka kwenye folder la Huawei Hilink Driver ulilodownload kulingana na bit ya windows yako X86 au X64

G. Chagua Driver yenye jina la ewser2k.inf kisha bonyeza Open

H. Bonyeza kwenye Huawei Incorporated >>> bonyeza Huawei Mobile Connect – 3G PC UI Interface kisha bonyeza Next italeta Update Driver Warning. Bonyeza Yes

I. Baada kumaliza kuinstall, utaletewa ujumbe wa Windows has successfully updated your driver software. Bonyeza Close

J. Itaonekana kama hivi



No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.