Jinsi ya kuhamisha mafile kutoka kwenye simu-computer au computer-simu bila kutumia USB Cable


Njia hii haitumii internet ili uweze kuhamisha mafile zako kutoka kwenye simu kwenda kwenye computer au kutoka kwenye computer kwenda kwenye simu wala USB cable yoyote. App hii inafanya kazi pia kuhamisha mafile  kwenye simu na simu. Kwa kutumia njia hii utaweza kuhamisha file lenye ukubwa wowote ule unaotaka

Mahitaji

Download Xender apk

1. Fungua Xender yako. Bonyeza kwenye picha ya paka juu kushoto mwa Xender


2. Bonyeza More


3. Bonyeza Connect to PC


4. Bonyeza kwenye kiduara chekundu (namba 5) kama inavyooneka kwenye picha chini

5. Itafungua Wifi Hotspot kwenye simu yako. Hii haimaniishi itatumia Mb zako. Zima Data kabisa.


6. Connect wifi kwenye computer yako.


7. Fungua browser yako, inaweza kuwa Mozilla, Chrome, Edge na zingine. Kwenye Address bar ya browser yako andika hiyo address uliyopewa kwenye Xender, inayoanzia  http://192.168.43.1.33455 na kisha ubonyeze Enter


8.  Bonyeza Accept kwenye simu yako


9. Itafunguka browser yako na itaonekana kama hivi.


10. Kutuma file kutoka kwenye computer kwenda kwenye simu. Bonyeza kwenye neno upload File.


11. Chagua file unalotaka kuhamisha inazaweza kuwa muziki, video, apps n.k kisha bonyeza Open. 


12. Utaliona file kwenye simu yako

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.