Jinsi ya kuongeza size ya partition kwenye computer bila kufuta data zilizomo

Hii ni software itakayokuwezesha kufuta, kuongeza au kupunguza ukubwa  wa partition ya hard disk kwenye computer yako. Hii ni njia rahisi sana na haichukui hata dk 10 kufanya Parttition kwenye computer yako. 

Mahitaji

Download MiniTool Partition


A. SPLIT

Unagawa Partition yako yaani unatengeneza Partition nyingine kupitia  partition mmoja. Kama ni chungwa unaligawa kulingana na ukubwa wa hilo chungwa. Unaweza kugawa mpaka Partition nne kulinga na ukubwa wa hard disk yako

B. EXTEND

Unaongeza ukubwa wa partition kupitia Partition zingine. Mfano Parttion yako ina ukubwa wa 2GB sasa unataka kuongeza mpaka ifike 56GB au 250GB. Ukubwa huu unapatikana kwa kumega kutoka kwenye Partition zingine. 

C. MERGE

Ni kuiambatanisha Partition mmoja na nyingine kuifanya iwe mmoja yaani unaiunganisha inakuwa mmoja

D. MOVE/RESIZE

Unahamisha Partition yako kwenda kwenye Partition nyingine na kuifanya kuwa mmoja. Unatakiwa utoe data zako kabla ya kufanya Move/resize kwasababu zitafuta data zako zote

Fuata hatua hizi ili uweze kuongeza ukubwa wa  partition kwenye computer yako bila kupoteza data

1. Fungua software yako. Kisha right click kwenye Partition unayotaka kuongeza ukubwa. Kisha bonyeza kwenye neno Extend


2. Chagua Partition unayotaka kupunguza ukubwa

3. Tumia mchale kuongeza au kupunguza ukubwa kutoka kwenye Partition unayotaka kumega. Kisha bonyeza OK


4. Bonyeza Apply. Subiri kama dakika kadhaa hivi itakuwa imemaliza 


No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.