Jinsi ya kuunlock modem ya E303h-1 Hilink

Hii ni modem ya Tigo  ambayo imefungwa ili uweze kutumia mtandao mmoja tu kwenye kifaa chako. Usitumie njia hii kufungua modem ya 303h-1 Hilink ambayo siyo ya mtandao wa Tigo. Hii njia ni kwa ajili ya Modem ya Tigo tu. Unlock e303h-1 Hilink

Mahitaji

Download Universal MasterCode
Download E303Hilink

Hatua kwa hatua namna ya kuunlock modem ya 303h-1 ya Tigo

1. Chomeka modem yako kwenye computer, install na uifunge. Weka laini tofauti na ya mtandao husika

2. Fungua universal Master Code.  Bonyeza kitufe cha Huawei, weka IMEI namba ya Modem yako (Funua mfuniko wa modem yako utaziona IMEI). Kisha bonyeza kitufe cha Calculate ili kupata flash code.



3. Extract 303H  na ui-run kwenye computer yako. Itakuomba password. Weka za Flash code na kisha bonyeza OK



4. Subiri mpaka imalizike. Usiiguse maana utaharibu modem yako. Kisha bonyeza Finish


Mpaka hapa utakuwa umshamaliza kuunlock modem yako


No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.