Jinsi ya kuunlock modem ya E303s-1 Tigo itumie mitandao yote

Kwa njia hii utaweza kuunlock modem zote za E303s-1 ya mtandao wa Tigo na za mitandao mingine. Unlock Huawei e303s-1 

Mahitaji

Download Universal MasterCode
Download E303S Unlocked Firmware

Hatua za kufuata ili kufungua modem ya E303s-1 ya Tigo na zingine uweze kutumia mitandao mingine.

1. Chomeka modem yako kwenye computer, install na kisha ufunge dashboard ya modem yako. (weka laini tofauti na ya mtandao husika)

2. Fungua universal unlock,  Bonyeza kitufe cha Huawei, weka IMEI namba ya Modem yako (funua mfuniko wa modem yako utaziona IMEI). Kisha bonyeza kitufe cha Calculate ili kupata flash code.


3. Extract E303S unlocked firmware kwenye computer yako. Itakuomba password. weka za Flash code

4. Subiri mpaka imalizike. Ikimalizika, chomoa na chomeka tena modem yako.Mpaka hapo utakuwa umeweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka. Enjoy



No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.