Njia salama ya kufuta Data zako kwenye Computer, Hard Drive, Flash Drive na Memory Card

Sasa hivi kumekuwepo na lindi la Data recovery sofware ambazo hutumika kurudisha data zilizofutika kwenye vifaa mbali mbali. .Hebu chukulia una taarifa muhimu unataka kuzifuta na hautaki mtu yoyote aje azione hizo taarifa. Baada ya kufuta kwa njia ya kawaida, baada ya siku kadhaa unazikuta kwenye social media. Utajisikiaje?
Tumia hizi software ambazo hufuta kwa kuweka key maalumu ambazo huwa ni vigumu kwa data recovery yoyote ile  kurudisha taarifa zako. Unapofuta Data zako huwezi tena kuzirudisha kwa kutumia Data recovery software au tool yoyote ile 

Fuata hatua hizi ili uweze kufuta data zako kwenye computer, hard drive, flash drive na memory card (SD Card)

NJIA YA KWANZA

Download Cclearner na install kwenye computer yako. Fungua software yako, bonyeza Tool, Drive Wiper, chagua kifaa chako kisha bonyeza wipe


NJIA YA PILI

1. Download Minitool Partition Wizard na install kwenye computer yako. Fungua software yako kisha right click kwenye hard drive au Memory Card (SD Card) unayotaka kufuta data zako. Bonyeza Wipe partition


2. Bonyeza OK. Kisha Bonyeza Apply

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.