Jinsi ya Kutatua Tatizo la Blog Kutopatikana Kwenye Search Engine ya Google na Bing

Kuna tatizo la jina la blog kutopatikana kwenye search engine ya google. Mwingine anaweza fikiri imefungwa baada ya kushare kwenye mitandao ya kijamii lakini jibu hakuna. Hakuna mtu anayeweza kufunga au kufuta blog yako isipokuwa Google au wewe mwenyewe.

Sababu

-Kupost vitu vinavyokiuka maadili ya nchi kulingana na sheria ya nchi wameamua kuifunga
-Kupost article zinaleta uchochezi au vurugu kwenye ambapo inaweza hatarisha vita kwenye nchi fulani
-Kuwachafua watu, kuwatukana viongozi wa dini, wa nchi, wasanii n.k
-Kutumia email zaidi ya moja kuingia kwenye blog yako. Umetumia email ya janjamwanduko@gmail.com kutengenezea blog yako lakini unapoingia kwenye blog yako unatumia makwanjidumila@gmail.com
-Kupost software zenye virus au zenye kuchukua taarifa za watu kwa lengo la kuhatarisha vifaa vya watu kama simu, computer, Tablet n.k

Jinsi ya kutatua tatizo la Blog kutopatika kwenye search engine ya Google na Bing.

NJIA YA KWANZA

Google Webmasters

1. Ingia kwenye website ya Google Webmasters kusubmit url ya blog yako kisha bonyeza Start now. Itakuomba email na password weka kisha bonyeza Next. Chagua URL Prefix, Andika url ya blog yako mfano https//www.agath64a.blogspot.com. Bonyeza Continue




2. Chagua HTML Tag. Kisha Copy the Meta tag na paste kwenye blog yako



3. Ingia kwenye blog yako. Bonyeza Theme, kisha Edit HTML



4. Bonyeza Ctrl+F kwenye keyboard ya computer yako. Itatokea Search bar andika <head kwenye search bar na kisha bonyeza enter. Paste meta tag yako chini ya <head. Bonyeza Save theme. 



7. Rudi kwenye Google Webmaster kisha bonyeza verify. Hatua namba 2


Bing Webmaster Tool

1. Ingia kwenye website ya Bing Webmaster Tool. Sign up kwa email yako na password. Kisha andika url ya blog yako na bonyeza Add



2. Andika url na sitemap kama inavyoonekana kwenye picha chini. Futa http:// na weka url ya blog yako https://agath64a.blogspot.com



3. Copy Meta tag


4. Ingia kwenye blog yako. Bonyeza Theme, kisha Edit HTML.  Bonyeza Ctrl+F kwenye keyboard ya computer yako. Itatokea Search bar andika <head kwenye search bar na kisha bonyeza enter. Paste meta tag yako chini ya <head. Bonyeza Save theme. 



5. Rudi kwenye Bing Webmaster Tool na bonyeza verify. Hatua namba 3. Blog yako itaonekana kama hivi



NJIA YA PILI

Hii njia inafanya kazi 100%. Kama bado haijaonekana blog yako kwenye search engine ya Google na Bing. Badilisha email kwenye blog yako. Jinsi ya kubadilisha au kuongeza email kwenye  blog  yako