Jinsi Ya Kubadili Email Kwenye Blog Yako

Kuna wakati unataka kubadilisha email uliyotumia kutengenezea blog kwasababu zako binafsi au unataka kuweka usiri ili watu wasikujue wewe ni nani.

Fuata hatua hizi ili uweze kubadilisha au kuongeza email kwenye blog yako (Jinsi ya kubadilisha au kuongeza email kwenye blog yako)

1. Ingia kwenye blog yako. Click on settings, kisha basic. Scroll down mpaka kwenye kipengele cha Permissions, Blog Authors na kisha Add Authors


2. Kwenye kibox cha Add authours. Andika email kisha bonyeza invite authors. Hapa unaweza kuweka email za zaidi ya watu 10


3. Kwenye blog yako itaoneka hivi


4. Ingia kwenye email yako. Fungua email utaona link yenye maneno Accept invitation. Bonyeza hapo


5. Bonyeza Accept invitation


6. Mpaka hapa utakuwa umeweza kubadilisha email kwenye blog yako. Unaweza kuweka Admin kama unataka blog yako itumie email mbili. Kama hautaki weka Author. Kama unataka ualike watu wawe wanapost kwenye blog yako waweke kama Author hivyo anakuwa hana mamlaka kubadili chochote kuhusu blog yako. Unaweza kutoa email kwa kubonyeza alama ya x


1 comment:

Note: Only a member of this blog may post a comment.