Jinsi Ya Kutengeneza Channel Ya Youtube Bure

Ili uweze kulipwa kwenye Youtube channel yako lazima u-apply monitazation (Ujiunge na Google Adsense)

Google Adsense ni kampuni ya matangazo ambayo hutumika kuwalipa watu wenye Forum, Blog, App (Admob), YouTube au Website kwa njia ya matangazo. Baada ya kujiunga na  Adsense itakupa code na utaweka kwenye blog au website yako kwahiyo matangazo yataanza kuonekana kwenye site
yako kwahiyo mtu akibonyeza tangazo utaweza kulipwa kwa mfumo wa USD na utaweza kupokea hela yako kupitia Western Union, Paypal, Payoneer au njia zingine za kupokelea pesa.

Kumbuka Google Adsense ya YouTube inajitegemea haingiliani na ya website, blog au Forum. Ya App inaitwa Admob. Jinsi ya kutengeneza blog bure kwa blogger

Adsense inalipa kwa mfumo wa impression (CPM) ya idadi ya watu 1000 watakaona tangazo kwenye channel yako ya YouTube. Wanalipa Dollar 0.5 hadi 1 kwa impression ya watu 1000 kutoka Tanzania waliona Tangazo lako. Mfano umepata view 100,000 waliona tangazo na CPM yako ipo fixed kwa 1

1000= 1 USD
100,000= 100 USD
Kwahiyo kwa watazamaji 100,000 walioangalia Tangazo utapata USD 100
USD 100 ndiyo kiwango cha kuomba pesa kutoka Google Adsense. Hakuna ulazima wowote wa kuwa na account bank ili ulipwe na Google, utatumia Western Union

Masharti ya kujiunga na Google Adsense

- Uwe na watch time hours 4000 and 1000 Subscribers
- Lazima channel yako iwe na Views 10,000 na kuendelea
- Uwe umeverify chanel yako kwa njia ya simu
- Uwe kwenye nchi zinazokubalika kupokea malipo ya YouTube

Muhimu

Epuka kuweka video za watu wengine yaani usi-copy na ku-paste. Jitahidi utengeneze video zako. Kama utacopy video na kuiweka kwenye chanel yako na hiyo video ina hati miliki kwahiyo pesa itakuwa inaenda kwa yule mwenye video. Kama utachukua video kutoka mtandaoni ifanyie editing kwanza kabla haujaipost kwenye chanel yako ya YouTube.

Epuka kuweka video zitakazokiuka maadili maana utafungiwa channel. Lugha unaweza tumia yoyote. Weka content za kuvutia zikazowavuta watazamaji kuangalia channel yako. Zinaweza kuwa zinahusu

        - Games
- Udaku
- Teknolojia
- Vichekesho
- Video za watoto kama masimulizi ya hadithi, katuni n.k
        - Movies au series (Movie zilizopo, zitakazo toka)
        - Matukio ya kushangaza
        - Utamaduni (Unaweza kuandika Documentary inayoelezea utamaduni wa jamii fulani)
        - Mpira
        - Mapishi
        - Urembo na Vipodozi
        - Mitindo ya nguo
        - Habari (Epuka kuripoti habari bila kufanyia utafiti)

Jinsi ya kutengeneza account / channel ya Youtube bure

1. Ingia YouTube, kisha Sign in kwa email yako kama hauna tengeneza email yako. Bonyeza Settings.



2. Bonyeza Create a new channel



4. Kwenye Brand Account name, andika jina la Youtube channel yako. kisha bonyeza Create. Fuata maelekezo mengine ili uweze kutengeneza account yako ya Youtube



Jinsi ya kufuta Channel / account ya Youtube 

Ingia Youtube. Angalia mkono wa kushoto,  shuka chini utaona neno Setting. Bonyeza Settings kisha Advanced setting >>> Delete channel



Jinsi ya kufuta video kwenye account / channel yako ya Youtube

1. Ingia kwenye Youtube video studio. Select video unayotaka kuifuta. Bonyeza kwenye neno Public, itakuletea menu, bonyeza Delete na hapo utakuwa umefanikiwa kuifuta video yako.



Mpaka hapo utakuwa umefankiwa kutengeneza channel yako ya YouTube

4 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.