Mambo ya kuzingatia blog yako iwe kwenye ukurasa wa kwanza wa Google

ili Kufanya blog yako ionekane ya kwanza au ya pili kwenye ukurasa wa google ni jambo rahisi ila unahitaji muda na kutuliza akili. Unatakiwa uwe mbunifu katika kuandaa makala (Articles) zako na pia kuifanya blog yako kuwa ya kwanza kwenye search engine ya Google.

Mambo muhimu yatakayokufanya blog yako ionekane ya kwanza kwenye Search engine ya Google. Jinsi ya kupata watembeleaji (traffic) wengi kwenye blog yako. Namna ya kufanya blog yako ionekane ya kwanza kwenye ukurasa wa Google

1. Andika Vichwa vya habari za post zisizofanana na za blog zingine

Hakikisha vichwa vyako vya habari havifanani na za kwenye blog nyingine kwasababu Google search engine huwa hai-scrawl post zenye kufanana vichwa vya habari. Ili kuepuka kuandika vichwa vya post vinavyofanana ingia kwenye Google andika kichwa cha habari. Hapa utaweza kuedit title yako kulingana na vichwa vya posts vilivyojitokeza. Download hiki kitabu 300 Power Headlines PDF kitakusaidia sana katika kuandika vichwa vizuri.



2. Content

Andika content zinazotatua matatizo ya watu kwa kuzingatia Keyword (Ni maneno yanatumiwa sana na watu kutafuta taarifa mbalimbali mtandaoni). Mfano maneno kama microsoft office 2019, Windows 10, kuroot simu, Matokeo ya kidato cha nne 2019, Mkopo, Kumake money online n.k Weka na miaka pia kama inawezekana. Ili kupata keyword zinazotrend ingia  Google suggests, Google keywords planner, lsi graph, Google related searches na wikipedia. Ukishajua ni keyword zipi zinazotrend andika article yako. Blog yako haitakosa kwenye ukurasa wa kwanza wa Google. Mfano. Ukiandika neno Jakaya Kikwete, Neno hili litajitokeza kwa kila blog, Forum au website lenye neno Jakaya Kikwete. Kwahiyo hapo lazima upate watembeleaji. 
Uwe na Content ambazo haujacopy sehemu yoyote na zenye maneno kuanzia 2000 na kuendelea Post au Article yako mmoja iwe na maneno kuanzia 2,000

Zingatia Niche usiandike ili mradi umeandika. Unataka kujishughulisha na nini kilimo & ufugaji, Technolojia, Ajira, Habari n.k. hii itakusaidia usiishiwe cha kupost

2. Tumia Backlinks

Backlinks ni kushare link yako kwenye mitandao ya kijamii na mitandao mingine. Hii itasaidia kupata watembeleaji wengi kupitia link yako. Watembeleaji wakiwa wengi itasaidia kuwa ya kwanza

3. Kushare post zako kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Jamii forum (JF), Instagram n.k
Hii mitandao ina nguvu sana. Unapotafuta kitu mtandaoni lazima ziionekane kwenye ukurasa wa kwanza wa Google kwahiyo kama umeshare post zako ni rahisi kuonekana. Inatakiwa uwe makini unaposhare maana kuna mitandao mingine wanakupiga ban.

Tumia Facebook page kushare post za blog yako kwenye magroup ya Facebook. Kwa kila account mmoja ya Facebook inakuwa na Page mmoja ambayo utaitumia kushare kwa Group 8 kila siku na utapost article 1 baada ya dakika 40 ili kuepuka kufungiwa.

4. Tumia Wikipedia, Quora na Pinterest

Ukipin Picha ya blog yako na link kwenye Pinterest kwa article inayotrend lazima upate watembeleaji wengi. Pia Fanya hivyo Quora na post wikipedia. Hapo lazima blog au website yako iwe ya kwanza.

5. Kuwa wa kwanza kupost habari zinazotrend. Kuwa wa kwanza kupost habari au tukio lilitokea hivi karibuni. 


6. Design vizuri blog yako iwe na muonekano mzuri



Design vizuri blog yako na weka menu bar na tumia template nzuri. Hii itasaidia sana kuongeza watembeleaji na kuwa ya kwanza kwenye ukurasa wa kwanza wa Google. Angalia mfano wa agath64a

Important Notice
Hakuna kitu kipya duniani cha kusema uandike ila kinachotakiwa ni ubunifu. Andika kwa kuangalia Keyword na mambo gani watu wanapenda sana kutafuta mitandaoni. Hii itafanya blog yako ifanye vizuri kwenye Search Engine Optimization (SEO). Utapata organic traffic (Traffic inapatikana kutoka kwenye SEO yaani mtu anapotafuta taarifa kupitia Google Search Engine au Bing.

1 comment:

  1. Mimi nataka kuweka wimbo watu wa download lakini nashindwa naomba unisaidi yaani nikipost wimbo na wa wau download inakuwaje

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.