Jinsi ya kuenable na kudisable write protected kwenye flash drive na Memory Card


Kuweka write protected kwenye flash drive au memory ni muhimu kama unahitaji data zako zisiliwe na virus, kubadilishwa au kufutwa kwahiyo ukishaweka data zako zitakuwa salama na hakuna mtu atakayeweza kufuta au kubadilisha taarifa zako.

Jinsi ya ku-enable write protection kwenye flash drive na Memory card

1. Bonyeza window button + X, bonyeza Command prompt (Admin)

2. Itafunguka command prompt as administrator


Andika haya maneno

- Diskpart bonyeza Enter
- List disk bonyeza Enter. Chagua disk unayotaka kuiwekea write protected. Yangu ni 1
- Select disk 1 bonyeza Enter
- Attribute disk set readonly bonyeza Enter
- Exit bonyeza Enter
Mpaka hapa utakuwa tayari umeshaweka write protected kwenye flash drive au memory card yako

Jinsi ya kuondoa write protected kwenye flash drive au memory card

- Diskpart bonyeza Enter
- List disk bonyeza Enter
- Select disk 1 bonyeza Enter
- Attribute disk clear readonly

Mpaka hapa utakuwa umeweza kuondoa write protected kwenye flash drive au memory card yako

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.