Zuia Copying, Editing na Printing kwenye PDF File
Kwa kutumia njia hii, utaweza kuzuia kazi zako, watu wasiweze kucopy, kuedit, kuibadilisha na kuiweka katika format nyingine au kuprint. Mtu yoyote ataweza kusoma kwenye kifaa chochote bila kuombwa kuweka password ila akitaka kuedit, kuprint, na kuibadilisha itamuomba password
Umetumia muda mwingi kuandika makala yako au kitabu na ukikiweka kwenye PDF lakini kuna watu watuchukua kazi yako na kuedit, kubadilisha kwenda kwenye Doc au kuprint na kuifanya kama ya kwao kwasababu watakuwa wameondoa taarifa muhimu na kuifanya kama yao.
Utaweka password kwenye PDF File na mtu akitaka kuedit itamlazimu aweke password. Hivyo hivyo hata kuprint. Njia hii ni rahisi na pia itakusaidia kulinda kazi zako ulizoziandika na kuziweka kwenye PDF File
Post a Comment