Namna ya kuunlock router R6601 Halotel Tanzania itumie mitandao yote


Hii ni router ya kampuni ya Halotel ambayo inatumia laini ya mtandao mmoja tu ambayo ni Hatolel. Huwezi kutumia SIM Card ya mtandao mwingine kwenye hii
router isipokuwa laini ya Halotel tu.
Kwa kutumia njia hii, utaweza kuunlock router yako ya Halotel Tanzania R6601 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.

Mahitaji
- ZTE Drivers
- Halotel R6601 Unlocked Firmware
- Halotel Flash tool

Jinsi ya kuunlock Router R6601 Halotel Tanzania 
1. Install ZTE drivers kwenye computer yako ili router yako R6601 iweze kutambuliwa. Unatakiwa uangalie computer yako inatumia Windows yenye bit X32/86 au X64. Kama unatumia X32/86 bit endelea kuinstall drives ila kama unatumia X64 bit inabidi u-disable driver signature enforcement kwenye computer yako. Baada ya kudisable, endelea kuinstall kama inavyoonyesha
kwenye hiyo video hapo juu

2. Run Halotel Flash tool, Bonyeza kwenye Scatter/Config file kisha chagua Halotel R6601 unlocked firmware kisha bonyeza open. Bonyeza Download button
3. Iweke router yako kwenye download mode. Washa router yako ikiwa haina laini yoyote, bonyeza button ya power on/off, itawaka taa nyekundu
4. Chomeka router yako kwenye computer kwa kutumia USB cable 
Iache mpaka imalize, ikimaliza italeta kibox chenye alama ya kijani. Ina maanisha hatua zote zimekamilika na router yako R6601 itakuwa unlocked na utaweza kutumia laini ya mtandao wowote ule unaoutaka. 

Chomoa router yako, weka laini ya mtandao wowote unaoutaka. Endelea kufurahia maisha 

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.