Software Muhimu Lazima Utumie Kwenye Computer Yako
1. Window 10 pro
Hii ni OS yenye feature nyingi sana ambayo naweza kuinstall app kama Facebook, iTunes, Instagram, Linkeldin, VlC, Speed test na apps zingine kupitia window store. ina Google drive, email, ina strong antivirus ambayo hautaji kuweka antivirus nyingine. Tumia Windows 10 yenye search bar ya Mic. Ili uweze kudownload apps unatakiwa unainstall Direct X kwanza kwenye computer yako
2. Microsoft Office 2019.
Hii ina feature nyingi sana kuliko zote. Nafanya vitu vingi kupitia Microsoft office 2019
3. Revo Uninstaller au Iobit uninstaller
Hizi zitakusaidia kutoa program na masalia yake. Ukiwa na program inakataa kutoka, tumia hizi software
4. Hetman internet spy
Hunisaidia kurecord kitu chochote nikifanyacho kwenye internet pamoja na kuhifadhi password
5. uTorrent
Hutumika kudownload software, movie and video kwenye torrent site
6. Internet Download Manager (IDM)
Hunisaidia kudownload file mbalimbali mtandaoni kwa urahisi zaidi na kwa speed kubwa kutoka kwenye website yoyote ile
7. Firefox au Google Chrome
Firefox huwa natumia kubrowse tovuti zilizokwenye freebasics.com ila kwa kuperuzi huwa natumia Google chrome kwasababu iko haraka kuliko browser zingine
8. Wondershare PDF element 6 pro
Hii ina feature nyingi sana mmoja wapo ni kusoma pdf file, kuconvert pdf kwenda kwenye format mbalimbali kama vile picha, docx, kuemerge pdf, na kuedit PDF file na pia kama ulisoma kitabu, basi siku ukianza kusoma utaanzia paleple na haina haja ya kutafuta pdf yaani wewe fungua hiyo program utaikuta kitabu chako kwenye page uliyoishia kusoma. Pia kuna Sumatra PDF Reader nayo ni nzuri sana
9. Cambridge Advanced dictionary
Katika software ambayo hutakiwi kukosa ni hii dictionary.
10. Mobile Partner
Hunisaidia kupiga simu, kujaza salio na kutuma meseji kwenye computer
11. Minitool Partition
Kwa ajili ya kufanya Partition na kufuta data kwa usalama wa taarifa zangu
12. Media player
AIMP kwa ajili ya kuplay audio
AllPlayer ni media player ambayo ni nzuri sana kuliko zote maana ina zoom in na out (Ku-enable zoom in + na Zoom out -). Kama ulikuwa unaplay movie kwenye media player zingine inascratch basi tumia hii software. Huwa napenda sana kuangalia movie in full screen pia ina auto play yaani ukiplay video mmoja basi itaanza kuplay na video zingine yenyewe.
Kuna VLC ila huwa siikubali sana sababu haina feature kama za Allplayer
13. Kaspersky Antivirus
Hii ni ndiyo kiboko ya antivirus zote maana ina feature nyingi mbali na hiyo ina disinfection feature ambayo husaidia kurudisha software au data zilizoliwa na virus katika hali yake ya kawaida
14. Easeus Data Recovery Software
Hutumika kurudisha data pale zilizofutwa kwa bahati mbaya kwenye computer au zilizoliwa na virus. Kuna kipindi unaweza kuhamisha data zako kwenye corrupted flash drive au memory hasa hizi fake huwa baadhi ya audio, picha, video au hazisomi hivyo natumia Easeus Data recovery.
15. Audio shell
Hii ni software ambayo hutumiaka kuondoa audio au video cover kwenye wimbo au video yoyote ile. Jinsi ya kuondoa video cover au audio cover
Post a Comment